Numbers 26:57-62

57 aHawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao: kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni;
kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;
kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.

58 bHizi pia zilikuwa koo za Walawi:
ukoo wa Walibni;
ukoo wa Wahebroni;
ukoo wa Wamahli;
ukoo wa Wamushi;
ukoo wa wana wa Kora.
(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu;
59 cjina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Haruni, Musa na dada yao Miriamu.
60 dHaruni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.
61 eLakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)

62 fWanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.

Copyright information for SwhKC